Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametoa wito wa kuwajibishwa pande zote zinazohuusika na mzozo wa Sudan, na kusisitiza haja ya kumalizwa vita na kutotosheka kuhesabu ukatili na uhalifu unaofanyika.
Amina Mohamed mesema katika mahojiano maalumu na televisheni ya Al-Jazeera kwamba: "Wahusika wote kwenye mzozo wa Sudan wanapaswa kuwajibishwa. Suala hili halipaswi kunyamaziwa kimya. Hata hivyo, lazima tukomeshe ukatili unaofanyika."
Afrisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza udharura wa kumomeshwa vita nchini Sudan na kuhudumia raia wanaokimbia makazi yao kutokana na vita.
Amina Mohammed alisisitiza kuwa suala la kusitishwa vita mara moja ni moja ya malengo ya juhudi za kieneo na kimataifa, sambamba na kuanzisha njia ya misaada ya kibinadamu na kufanyika mazungumzo ya kurejesha amani nchini Sudan.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia amepongeza juhudi zinazofanywa na Umoja wa Afrika, jumuiya ya IGAD na Umoja wa Mataifa katika jitihada za kusitisha mapigano nchini Sudan.
Amesema hali ya sasa ya Sudan ni "mgogoro mkubwa na wa kutisha," akifafanua kuwa, idadi ya wakimbizi ni kubwa na kwamba hospitali hazitaweza kuwashughulikia. Wakimbizi wa Sudan
Kwa upande wake, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema takwimu za Shirika la Kimataifa la Wahajiri zinathibitisha kwamba, watu milioni mbili na laki sita wamekuwa wakimbizi ndani ya Sudan tangu kuanza kwa mzozo huo, huku idadi ya wale waliovuka mipaka na kwenda nchi jirani wakifikiwa watu laki 7 na 30 elfu.