Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Tumejitolea kuvipa vikosi vya Somalia mafunzo ya kiufundi na kiusalama

Au Au Somalia Kusepa.jpeg UN: Tumejitolea kuvipa vikosi vya Somalia mafunzo ya kiufundi na kiusalama

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Misaada ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia (UNSOS) ambayo imekuwa ikiisaidia kikamilifu Somalia katika kuimarisha uwezo wa vikosi vyake usalama imetangaza kuwa imejitolea kikamilifu kuvipa mafunzo ya kiufundi vikosi vya kulinda usalama wa ndani ya nchi hiyoi ya Pembe ya Afrika wakati huu wa kipindi cha mpito.

Ofisi ya UNSOS ambayo inatoa msaada wa vifaa kwa Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imesema katika taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumamosi katika mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu, kwamba mafunzo hayo yatahusiana na uendeshaji na ufundi endelevu wa vifaa kwa ajili ya usalama.

Afisa Msimamizi wa UNSOS, Qurat-Ul-Ain Sadozai amesema kuwa, "Sisi UNSOS, dhamira yetu ya kukikasaidia kikosi cha ATMIS na serikali ya Somalia inabakia kuwa thabiti."

ATMIS na UNSOS zote zilitangaza kukamilika zoezi la awamu ya pili la kuondoa vikosi vya kigeni nchini humo imehusisha kupunguzwa idadi ya askari 3,000 wa kigeni nchini humo. ATMIS ilikabidhi vituo saba vya kijeshi kwa serikali ya Somalia na kufunga vingine viwili.

Vikosi vya ATMIS nchini Somalia

Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Somalia Hussein Sheikh-Ali ameupongeza Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Mataifa na washirika wa kimataifa kwa kujitolea kwao kutafuta amani na usalama nchini Somalia.

Sam Okiding, Kamanda wa Kikosi cha ATMIS alisifu kazi ya kipekee ya pamoja ya kamati ya utatuzi - ATMIS, serikali ya Somalia na UNSOS - kwa kukamilisha mafanikio ya Awamu ya Kwanza na ya Pili ya zoezi la kuondoka askari wa kigeni nchini humo.

Amesema: “Juhudi zetu za pamoja zimekuwa kubwa katika kupunguza jumla ya askari 5,000 katika awamu zote hizo mbili na hivi karibuni tutaanza maandalizi ya awamu inayofuata ya tatu ya kupunguza idadi ya askari wetu 4,000 mwezi Juni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live