Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Msako wa watetezi haki za binadamu Burundi unatisha

UN Burundi Burundi UN: Msako wa watetezi haki za binadamu Burundi unatisha

Thu, 23 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Kamishna wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema ina hofu kubwa juu ya ongezeko la msako dhidi ya watetezi wa haki nchini Burundi kufuatia kuswekwa korokoroni hivi karibuni kwa watetezi watano wa haki za binadamu na kufungwa jela kwa mwandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswi, msemaji wa ofisi hiyo Martha Hurtado ametaja watetezi hao walioko rumande kuwa ni Sonia Ndikumasabo, Marie Emerusabe, Audace Havyarimana, Sylvana Inamahoro na Prosper Runyange ambao walikamatwa tarehe 14 mwezi uliopita kutokana na kazi yao.

Mahakama ya Rufaa nchini Burundi tarehe 15 mwezi huu ilithibitisha hukumu ya Mahakama Kuu kwa watetezi hao kuendelea kusalia rumande wakisubiri kesi yao.

Kwa mujibu wa Bi. Hurtado, mashtaka dhidi ya watano hao ni uasi, kudhoofisha usalama wa ndani ya nchi na utendaji kazi wa sekta ya fedha ya umma. Watetezi watano wa haki za binadamu walioko rumande

“Mashtaka hayo yanaonekana kuhusishwa moja kwa moja na uhusiano wao na shirika la kimataifa la haki za binadamu, ‘Avocats sans Frontières’ au watetezi bila mipaka,” amesema Bi. Hurtado.

Amefafanua kuwa kufanya kazi na shirika lisilo la kiserikali hata kama halijasajiliwa nchini Burundi, sio kosa na haipasi kukatazwa chini ya sheria ya Burundi.

Ameongeza kuwa msako dhidi ya mashirika ya kiraia unafanyika huku wakishuhudia pia mashambulizi dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Burundi.

Msemaji wa Ofisi ya Kamishna wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ameendelea kueleza kuwa, msako dhidi ya mashirika ya kiraia unafanyika huku wakishuhudia pia mashambulizi dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari huko Burundi.

Bi Hurtadi ametolea mfano wa kisa cha Floriane Irangabiye, mwanahabari ambaye amesota gerezani kwa zaidi ya miezi sita kwa sababu ya kufanya kazi yake na kufafanua kuwa, Floriane alikamatwa mwezi Agosti mwaka jana baada ya safari yake nchini Rwanda kwa sababu ya mahojiano ya redio aliyofanya na Warundi wawili wanaoishi nje ya nchi. Watu hao ni mwanahabari mwenzake na mtetezi wa haki za binadamu.

Tarehe Pili mwezi Januari mwaka huu alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela na faini ya dola 500 kwa madai ya kudhoofisha mamlaka ya nchi.

Msemaji wa Ofisi ya Kamishna wa Haki za Binadamu wa UN amekumbusha kuwa ukandamizaji wa mashirika ya kiraia kwa misingi iliyo kinyume na wajibu wa kitaifa wa Burundi umekuwa unashamiri tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hali ambayo imesababisha watetezi wa haki za binadamu na wanahabari kukimbilia ughaibuni.

“Tunaisihi serikali ya Burundi izingatie kwa kina viwango vya haki za binadamu hususan kujielezea na kukusanyika na kuwaachia huru wale wote walioko ndani na mashtaka dhidi yao yafutwe,” amesema Bi. Hurtado..

Chanzo: www.tanzaniaweb.live