Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Mgogoro Somalia unaua maelfu!

Watu 6 Wauwawa, 10 Wajeruhiwa Katika Shambulizi Somalia UN: Mgogoro Somalia unaua maelfu!

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwakilishi wa umoja wa mataifa nchini Somalia, Catriona Laing, amesema mgogoro katika nchi hiyo unazidi kusabisha vifo vya maelfu ya raia wasiokuwa na hatia

Catriona ameliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba idadi ya raia waliofariki nchini Somalia mwaka uliopita kutokana na mzozo nchini humo ni juu zaidi tangu mwaka 2017, hili likihusishwa na magaidi wa kundi la Al Shabaab na mapigano yanayohusisha eneo lililojitenga la Somaliland.

Aidha Catriona anasema mwaka huu pekee raia 1, 289 wamafariki kutokana na migogoro hiyo.

Magaidi wa Al shabaab wamekuwa wakitekeleza mashambulio dhidi ya serikali nchini Somalia kwa zaidi ya miaka 15 sasa.

Licha ya magaidi hao kuondolewa kwa baadhi ya miji mikuu uwepo wao bado upo katika mitaa mbalimbali ya vijijini na juhudi za rais Hassan Sheikh Mohamu kuanzisha mapambano dhidi kundi hilo, hazijaonekana kuzaa matunda, ambapo pia wamekuwa wakitekeleza mashambulio kwa taifa jiani la kenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live