Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Mapigano Sudan yasababisha kuongezeka kwa wakimbizi duniani

Sudan Wakimbizi Wakimbizi.jpeg UN: Mapigano Sudan yasababisha kuongezeka kwa wakimbizi duniani

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu huko Sudan amesema kuwa mapigano yanayoendelea nchini humo yanapelekea kuongezeka haraka mgogoro unapanuka wa wakimbizi duniani.

Clementine Nkweta Salami amesema kuwa, kwa wastani, zaidi ya watu 30,000 wanakimbia makazi yao nchini Sudan kila siku. Clentina Nkweta Salami ameongeza kuwa katika halia mbayo nusu ya wakazi wa Sudan wanahitaji misaada ya kibinadamu na ulinzi, mgogoro unaoikabili nchi hiyo pia umedumaza sekta ya afya nchini huku asilimia 70 ya hospitali za Sudan zikiwa hazifanyi kazi. Clementine Nkweta Salami

Mjumbe Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu huko Sudan ametahadharisha pia kuwa, mapigano yanayoendelea Sudan yanaweza kuathiri pakubwa usalama wa chakula nchini humo.

Mapigano ya silaha yalianza huko Sudan Aprili 15 mwaka huu kati ya jeshi la nchi hiyo linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) chini ya uongozi wa Kamanda Hamdan Dagalo ambapo hadi sasa juhudi za upatanishi za kimataifa za kuhitimisha mapigano hayo na kuzishawishi pande hasimu kuketi kwenye meza ya mazungumzo zimegonga mwamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live