Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Majenerali hasimu wa Sudan sasa kukutana

Mapigano Yanaendelea Sudan Na Kusababisha Vifo Kwa Raia UN: Majenerali hasimu wa Sudan sasa kukutana

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mkuu wa jeshi nchini Sudan, Jenerali Abdel-Fattah al-Burhan na mpinzani wake ambaye ni kamanda wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), Mohamed Hamdan Dagalo, wamekubali kukutana kwa ajili ya mazungumzo kuhusu hali mbaya ya binadamu nchini humo.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia misaada ya binadamu Martin Griffiths amesema kuwa, siku chache zilizopita alizungumza na viongozi hao wawili lakini haijathibitishwa ni lini na wapi mazungumzo hayo yatafanyika.

Umoja wa Mataifa unatangaza habari hiyo katika hali ambayo, hadi sasa juhudi za kuwakutanisha majenerali hao wa kijeshi wa Sudan hazijafanikiwa huku hali ya kibinadamu katika nchi hiyo ikizidi kuwa mbaya siku baada ya siku.

Vita vya kuwania madaraka kati ya majenerali wa kijeshi vinandelea kuiangamiza Sudan huku taarifa zikisema kuwa Wasudan milioni 25 wanateseka kwa njaa kutokana na vita hivyo vya uchu wa madaraka baina ya majenerali hao wa kijeshi.

Jenerali Abdul Fattah Burhan, mkuu wa baraza la kijeshi ambaye pia ndiye kamanda mkuu wa wa jeshi la Sudan wiki iliyopita aliamuru jeshi na makundi yote yenye silaha kushambulia vikosi vya RSF sehemu yoyote vinapokutana navyo. Karibu watu milioni watu wamebaki bila makazi kufuatia vita vya ndani nchini humo

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianza huko Sudan Aprili 15 mwaka jana kati ya jeshi la nchi hiyo linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) chini ya uongozi wa Kamanda Hamdan Dagalo ambapo hadi sasa juhudi za upatanishi za kimataifa za kuhitimisha mapigano hayo na kuzishawishi pande hasimu kuketi kwenye meza ya mazungumzo zimegonga mwamba.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kibinadamu imetangaza kuwa zaidi ya watu 13,000 wameuawa na wengine 26,000 kujeruhiwa katika vita vinavyoendelea nchini Sudan tangu mwaka jana (2023).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live