Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Mafuriko ya Afrika Mashariki hutokea mara moja kwa karne

Mks Mafuriko UN: Mafuriko ya Afrika Mashariki hutokea mara moja kwa karne

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mafuriko ambayo yameathiri maelfu ya watu nchini Somalia na nchi jirani za Afrika Mashariki kuwa ni tukio la mara moja katika karne.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa walisema zaidi ya watu milioni 1.5 nchini Somalia wanaweza kuathiriwa na mvua kubwa ya msimu, ambayo imefanywa kuwa mbaya zaidi kutokana na athari za pamoja za matukio mawili ya hali ya hewa - athari ya El NiƱo na Dipole ya Bahari ya Hindi.

Mvua kubwa iliyoanza mapema Oktoba ilifuatia miezi kadhaa ya ukame mkali katika eneo hilo.

Zaidi ya watu 300,000 wamelazimika kuyahama makazi yao nchini Somalia huku miji na vijiji vikikumbwa na mafurika kaskazini mwa Kenya.

Taasisi za masuala ya kibinadamu za Umoja wa Mataifa zimesema kwamba zimetenga dola milioni 25 za Kimarekani kwa ajili ya kuanza kuwafikishia misaada wananchi walioathiriwa na mafuriko makubwa nchini Somalia.

Tayari watu milioni moja la laki mbili wameripotiwa kuathiriwa na mafuriko hayo ya mara moja kwa karne ya nchini Somalia.

Athari za mafuriko katika moja ya maeneo ya Somalia

Sehemu nyingine ya taarifa ya OCHA imesema: Somalia, ambayo kabla ya mafuriko hayo iliopitia kipindi kigumu sana cha ukame wa kihistoria, ni moja ya nchi nyingi ambazo zinatabiriwa kukumbwa na hatari kubwa ya mafuriko, ukame na joto kali katika miezi ijayo. Majanga hayo ya kimaumbile yanachochewa na vitu mbalimbali ikiwemo El Nino.

Kabla ya hapo Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) lilikuwa limetabiri kutokea mafuriko makubwa ambayo hayajawahi kutokea nchini Somalia katika kipindi cha karne moja yaani miaka 100 iliyopita na kusababisha maafa makubwa ya roho na mali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live