Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Idadi ya watu maskini kuongeza Afrika 2024

Umaskiniongezeko Afrika UN: Idadi ya watu maskini kuongeza Afrika 2024

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa idadi ya watu wanaoteseka kutokana na baa la njaa katikati ya Afrika na magharibi mwa bara hilo inatarajiwa kufikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa cha watu milioni 49 na laki tano ifikapo katikati ya mwaka ujao wa 2024.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Xinhua, Stephane Dujarric, msemaji mkuu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amenukulu Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF na Shirika la umoja huo la Chakula na Kilimo FAO yakieleza katika ripoti ya uchambuzi wao juu ya usalama wa chakula wa kikanda na kutangaza kwamba, idadi hiyo ya watu itafika katika kipindi cha kati ya mwezi Juni hadi Agosti mwakani.

Dujarric amebainisha kuwa, taasisi hizo tatu zinatoa wito kwa serikali na wafadhili wa kifedha kuweka kipaumbele kwa programu zinazoimarisha mifumo ya chakula na maisha inayohimili hali ngumu ya hewa na kuwekeza katika mifumo ya utoaji msukumo wa kijamii.

Taasisi hizo tatu za UN zimeripoti kuwa uchambuzi wao unaonyesha kuwa hali ya njaa inatia wasiwasi hasa katika nchi za maeneo ya pwani, ambapo idadi ya wanawake, wanaume na watoto wanaokabiliwa na njaa kali inatarajiwa kufikia watu milioni sita na laki mbili, ambayo ni ongezeko la 16% katika mwaka huu.

Kwa mujibu wa mashirika hayo, njaa kali katika eneo hilo inasababishwa zaidi na machafuko, athari za hali mbaya ya tabianchi na kuongezeka kwa bei ya mafuta na bidhaa za chakula..

Chanzo: www.tanzaniaweb.live