Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Idadi ya wakimbizi inaongezeka DRC

Wakimbizi Congo Drc.png UN: Idadi ya wakimbizi inaongezeka DRC

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mamilioni ya watu wameyakimbia makazi yao katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2023, watu milioni saba walikimbia makazi yao nchini DRC, wakiwemo milioni 2 na laki 5 katika jimbo la Kivu Kaskazini pekee.

Maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wanaishi katika kambi zisizo salama kiafya mashariki mwa nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na mzozo kati ya waasi na jeshi la nchi hiyo.

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, hivi sasa kuna wimbi jipya la wakimbizi katika baadhi ya maeneo ya Jamhuri ya Kidemokeasia ya Congo.

Wimbi jipya la wakimbizi limeibuka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuzuka mapigano mapya kati ya jeshi la nchi hiyo na kuundi la waasi la M23.

Mwezi uliopita wa Januari Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilitangaza kuanzisha operesheni ya pamoja na wanajeshi wa kikosi cha Jumuiya ya Maendelezo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC dhidi ya waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ilialika kikosi hicho cha SADC baada ya kusema kuwa haijaridhika na wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ambao walitakiwa kupambana na waasi wa M23.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikimtuhumu jirani yake Rwanda kuwa inaliunga mkono kundi la waasi wa M23, madai ambayo yamekanushwa na Kigali, lakini yanaungwa mkono na Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live