Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Hali ya usalama mashariki mwa DRC inazidi kuwa mbaya

Shambulizi La Kuvizia Lafanyika DRC UN: Hali ya usalama mashariki mwa DRC inazidi kuwa mbaya

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hali ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeendelea kuzorota katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita licha ya kutulia mapigano kati ya kundi la waaasi la Vuguvugu la Machi 23 (M23) na vikosi vya serikali katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Hayo yamesemwa na Bi Martha Pobee, msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Afrika ambaye ameongeza kuwa, ingawa hadi hivi sasa usitishaji mapigano kati ya kundi la waasi la M23 na vikosi vya serikali umeleta baadhi ya mafanikio lakini usalama unaendelea kuzorota katika maeneo hayo.

Amesema, zoezi la kuondoka waasi wa M23 katika maeneo unaliyoyateka na kuyakaliwa kwa mabavu linakwenda kwa kasi ya kinyonga na kuna ucheleweshaji wa makusudi unaofanyika kwa malengo ya kisiasa. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Aidha ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba: Waasi wa M23 bado wanadhibiti sehemu kubwa ya maeneo ya Masisi na Rutshuru pamoja na njia za usafiri wa watu na bidhaa katika maeneo hayo.

Amesema, hofu nyingine imejitokeza hivi sasa baada ya waasi wa M23 kuanza kujipanga upya katika wiki za hivi karibuni na kuzua hofu kwamba mapigano yanaweza kuzuka tena wakati wowote ule.

Amesema: "M23 inaendelea kusababisha ukosefu wa usalama, imeripotiwa kuwa wameua takriban raia 47 kwenye eneo la Kivu Kaskazini katika kipindi cha hivi majuzi."Vile vile Bi Martha Pobee amepongeza juhudi zinazoendelea za viongozi wa nchi za ukanda huo za kuzishawishi pande husika kutekeleza maamuzi ya ramani ya njia yaliyofikiwa mjini Luanda na Nairobi, akisisitiza kuwa, kikosi cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kinachojulikana kwa jina la MONUSCO, kitaendelea kuisaidia serikali ya Kongo katika juhudi za kurejesha usalama kwenye maeneo hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live