Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Chuki za kikabila zimekithiri nchini Sudan

Maelfu Wanatoroka Mauaji Mapya Ya Kikabila Huko Darfur Nchini Sudan UN: Chuki za kikabila zinashadidi nchini Sudan

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Sudan, Radhouane Nouicer, amesema kwa sasa baadhi ya makundi ya Sudan yanalenga watu wa makabila au makundi madogo, kitendo ambacho kinashamirisha kauli za chuki.

Bwana Nouicer amesema kitendo hicho ni miongoni mwa matukio ya ukiukwaji mkubwa wa haki za msingi za binadamu kwenye taifa hilo ambalo mzozo wake unakaribia kutimiza miezi 10 tangu uanze mwaka jana mwezi Aprili.

Mtaalamu huyo wa UN amesema kitendo hicho cha makundi mengine kushambulia makabila madogo “kinachochea kauli za chuki katika maeneo mengi ya nchi na ametaka hali hiyo isitishwe.”

Ameongeza kuwa “tumeshuhudia watu kuuawa kiholela, mashambulizi kwenye maeneo binafsi na ya kiraia, watu kuswekwa korokoroni kinyume cha sheria wakiwemo wanaharakati wa haki za binadamu na wawakilishi wa mashirika ya kiraia.”

Vitendo vingine ni watu kuteswa, vipigo, uporaji wa mali za umma na za watu binafsi, na vilevile kupatikana kwa makaburi walimozikwa watu wengi. Vita Sudan

Wakati huo huo Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kibinadamu imetangaza kuwa zaidi ya watu 13,000 wameuawa na wengine 26,000 kujeruhiwa katika vita vinavyoendelea nchini Sudan tangu mwaka jana,

Sudan ilikumbwa na vita kati ya Jeshi la Kitaifa, linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye ni mkuu wa Baraza Tawala la nchi hiyo, na kundi la wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) tangu Aprili 2023.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema katika taarifa yake kwamba, "Takriban watu milioni 7.6 wamekimbia makazi yao ndani na nje ya Sudan tangu mapigano yazuke

Chanzo: www.tanzaniaweb.live