Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Changamoto nyingi zinaathiri utoaji wa misaada ya kibinadamu Sudan

Utoaji Msaada Sudan UN: Changamoto nyingi zinaathiri utoaji wa misaada ya kibinadamu Sudan

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema kuwa, kuna changamoto nyingi zinazoathiri zoezi la kusambaza misaada ya kibinadamu katika maeneo mengi ya Sudan.

Katika taarifa yake, OCHA imezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa usalama, uporaji, vikwazo vya urasimu, mawasiliano mabovu, mitandao duni ya simu, ukosefu wa fedha na wafanyakazi wachache wa kiufundi na kibinadamu.

Kwenye taarifa yake nyingine, taarifa hiyo imesema: "Uhaba wa mafuta nao unaathiri harakati za wafanyikazi wanaosambaza misaada ya kibinadamu na vifaa na uzalishaji wa nishati inayohitajika katika kazi zao, ikiwa ni pamoja na usambazaji wa maji.

Licha ya changamoto hizi zote, lakini mashirika ya misaada ya kibinadamu yanaendelea kufanya kazi zao za kuokoa maisha ya watu walioko kwenye mazingira magumu kwa kadiri OCHA inavyoweza kuwafikia.

Ofisi hiyio vilevile imesema, Mpango wa Kukabiliana na Majanga ya Kibinadamu wa 2023 uliofanyiwa marekebisho kwa Sudan, umekuwa ukipata ufadhili kwa asilimia 40.8 tu hadi kufikia tarehe 4 mwezi huu wa Januari, 2024.

Sudan imekuwa ikishuhudia mapigano makali baina ya majenerali wa kijeshi wenye uchu wa madaraka wanaoongozwa makundi mawili, yaani Abdel Fattah al Burhan anayeongoza jeshi la Sudan na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo maarufu kwa jina la Hemedti anayeongozwa Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF katika mapigano ya kijeshi yaliyioanza tangu Aprili 15, 2023.

Katika ripoti yake ya mwezi uliopita wa Disemba, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilisema kuwa, zaidi ya watu 12,000 walikuwa wamethibitishwa kuuawa katika mapigano hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live