Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Baa la njaa kuendela kuikumba Afrika Mashariki

Njaa Tigray Baa la njaa kuendela kuikumba Afrika Mashariki

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashirika sita ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa masuala ya kibinadamu wametoa tahadhari ya baa la njaa kunyemelea eneo la Afrika Mashariki baada ya miaka minne ya ukame mkali huku ikitabiriwa uhaba wa mvua kwa mwaka mwingine wa tano mfululizo.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa mjini Nairobi Kenya na mashirika ya Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, la chakula na kilimo FAO, la kuhudumia watoto UNICEF, la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la utabiri wa hali ya hewa WMO na la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA pamoja na washirika wengine wa masuala kibinadamu imesema, Somalia na maeneo kadhaa ya Kenya na Ethiopia yameathiriwa na baa la hali mbaya ya ukame ambayo haijawahi kushuhudiwa kwa miaka 40 sasa, ambapo misimu minne mfululizo ya mvua imekuwa na kiwango cha chini sana cha mvua.

Taarifa hiyo ya pamoja imesema, zaidi ya watu milioni moja wamekimbia makazi yao Somalia na kusini mwa Ethiopia.

Upungufu wa maji uliopo umechochewa na hali mbaya ya joto la juu sana ambalo linatabiriwa kuendelea hadi msimu wa kiangazi wa Juni-Septemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live