Umoja wa Mataifa (UN) imetoa angalizo hilo katika ripoti yake kuhusu biashara haramu ya bidhaa za matibabu.
Biashara hiyo inaweza kusababisha dawa za kuua wadudu kutofanya kazi au maambukizi ya magonjwa hatari, pia kudhoofisha mifumo ya afya kwa watumiaji.
Kati ya Januari 2017 hadi Disemba 2021, tani 605 za bidhaa za matibabu zilikamatwa Afrika Magharibi katika operesheni za kimataifa, huku ikielezqa kuna vifo 267,000 kila mwaka vinavyohusishwa na matumizi ya dawa za malaria zisizokidhi vigezo.
Ofisi ya UN inayosimamia Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) imesema kuna kasoro kadhaa katika kuripoti kuhusu biashara hiyo haramu na huenda idadi ya dawa hizo zisizofaa ikiwa juu zaidi ya ilivyo kwenye takwimu.