Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Afrika inapaswa kuwa na mwakilishi katika Baraza la Usalama

Guterres Atoa Wito Kwa Israel Na Hamas Kuongeza Muda Wa Sitisho La Mapigano UN: Afrika inapaswa kuwa na mwakilishi katika Baraza la Usalama

Sun, 21 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelikosoa Baraza la Usalama la umoja huo kwa kutokuwa na mwakilishi wa kudumu kutoka Afrika. Guterres amehoji katika ukurasa wake wa X kwamba: "Je, tunawezaje kukubali kwamba Afrika haina hata mwanachama mmoja wa kudumu katika Baraza la Usalama?"

Amesema kuwa, taasisi lazima ziakisi ulimwengu wa leo, si ule wa miaka 80 iliyopita. Mkutano wa kilele wa mwezi Septemba utakuwa fursa ya kuzingatia mageuzi ya uongozi wa kimataifa na kujenga upya uaminifu."

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekariri takwa lake la kusitishwa vita haraka iwezekanavyo na kuachiwa huru mateka wote bila ya masharti huko Gaza.

Huku akiashiria hali ya kibinadamu Ukanda wa Gaza, eneo ambalo linashuhudia mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema: Watu katika Ukanda wa Gaza wanauawa si tu kwa kupigwa na mabomu na risasi pekee bali pia kwa kukosa pia chakula na maji safi, hospitali zisizo na huduma ya umeme na dawa za matibabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live