Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN, AU wataka Somali yenye nguvu

Afisa Wa Somalia Anaonya Mpango Wa ATMIS UN, AU wataka Somali yenye nguvu

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu za Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa nchini Somalia zimetilia mkazo msimamo wao wa kuunga mkono mchakato wa kujenga taifa lenye nguvu la Somalia.

Mohamed El-Amine Souef, mkuu wa Ujumbe wa Mpito wa AU nchini Somalia (ATMIS) na Aisa Kirabo Kacyira, Mkuu wa Ofisi ya Msaada wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia (UNSOS) wameutembelea mji wa Kismayo wa kusini mwa Somalia, ambako wamekutana na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wale wa timu ya Umoja wa Afrika ATMIS na kujadiliana nao vita vinavyoendelea vya kupambana na genge la kigaidi la al-Shabab pamoja na masuala mengine ya usalama na ya kisiasa.

Souef amewataka wafanyakazi hao kuendelea kutoa mafunzo maalumu na uzoefu na maarifa yao kwa watumishi wa umma wa Somalia ili kusaidia kuongeza idadi ya wafanyakazi wenye ujuzi katika sekta mbalimbali. Mwanajeshi wa Uganda katika operesheni ya kulinda amani ya AU nchini Somaliaa

Taarifa ya pamoja ya timu hizo mbili iliyotolewa mjini Mogadishu imesema: "Somalia imepata maendeleo makubwa, na maendeleo hayo yametokana na ushirikiano wa ATMIS na Umoja wa Mataifa katika kuimarisha usalama na mafanikio kwenye mapigano dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab.

Leo hii watu nchini Somalia wanaweza kuishi kwa usalama." Ziara ya viongozi hao timu hizo mbili za Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa imefanyika wakati ambapo ATMIS na washirika wake wanajiandaa kufanya tathmini ya pamoja ya kiufundi katika awamu ya kwanza ya kuondoka askari wa ATMIS huko Somalia na ambalo ilimaziki mwezi Juni mwaka huu. Katika awamu ya pili ya zoezi hilo, ATMIS itahitajika kuondoa askari wengine 3,000 hadi mwisho wa Septemba.

Kwenye awamu ya kwanza, ATMIS iliondoa wanajeshi 2,000 na kuvikabidhi vikosi vya ulinzi na usalama vya Somalia kambi sita za kijeshi zilizokuwa zikisimamiwa na kikosi hicho cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live