Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UDA: Ruto azidi kukumbwa na vizingiti kuelekea 2022

1569ba7213d42461 UDA: Ruto azidi kukumbwa na vizingiti kuelekea 2022

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Gari la DP Ruto limeanza kupata panchari hata kabla ya kuondoka kwenye safari ya 2022Tofauti zimeanza kuibuka miongoni mwa viongozi huku Kuria na Kiunjuri wakisema ni lazima waunde vyama vyaoRuto amekuwa akipigia debe viongozi wote kukaa ndani ya UDA ili wawe na nyumba moja yenye nguvuMasaibu yameanza kukumba kambi ya kisiasa ya Naibu Rais William Ruto kuhusu karata yake ya siasa za 2022.

Duru zinaarifu kuwa wanasiasa Mwangi Kiunjuri na Moses Kuria wamemwambia DP Ruto wazi kuwa hawawezi kujiunga na UDA.

Kwa mujibu wa wapekuzi, Kiunjuri ambaye ni kiongozi wa chama cha The Service Party na Kuria wa Chama cha Kazi, wawili hao wamekubali kumuunga DP mkono lakini wamesema hawavunji vyama vyao.

Kwa upande mwingine, viongozi kama vile Irungu Kang'ata nao wamesema hakuna haja ya wenzao kuunda vyama vya kimaeneo.

"Hakuna mtu anaweza kusema kuwa wana chama cha Kitaifa. Vyama vyote ni vya eneo fulani," Kiunjuri alisema.



"Kile tunataka si kutafuta muungano au chama cha kimaeneo ila kuunda na kujenga UDA. Lakini ni kweli kuna baadhi ya viongozi wa Mt Kenya ambao wansema wanataka chama cha eneo hili

"Sisi wa kutoka Murang'a hatuwezi kufuata hilo. Tunataka chama kimoja ili kuwaleta watu wote pamoja na chama hicho ni UDA," Kang'ata alisema.



Mbunge Kuria alisema Mt Kenya iko tayari kumuunga mkono DP Ruto lakini viongozi waachwa waunde vyama wanavyotaka.

"Tumekubali kuwa hatutakuwa na mgombea wa urais kwa mara ya kwanza katika miaka 30. Alafu tena utuambia kuwa hatuwezi kuwa na chama chetu? Hilo haliwezekani, na siogopi kutuwa nje ya serikali ya sasa ama ile ijayo," alisema Kuria.

Kuria alisema itakuwa vigumu kwa maslahi ya maeneo kuwasilishwa serikali bila ya vyama tanzu kwenye serikali hiyo.

"Vyama ndivyo nguzo ya uongozi. Kuna masuala ambayo ni lazima yapiganiwe na vyama vya eneo fulani," alisema Kuria.

"Hatubanduki, kwa hivyo tuzoeane mapema jamaa," Kuria aliongeza akisema kama hilo litaathiri uhusiano wake na DP hatajutia.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke