Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UDA: Nyumba ya DP Ruto yaanza kubomoka, toroli imekwama matopeni

Df56e5e15d80094b UDA: Nyumba ya DP Ruto yaanza kubomoka, toroli imekwama matopeni

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Toroli ya DP ilikwama kwenye matope na sasa waliokuwa ndani wameanza kuhepa

- Wadadisi walisema ni lazima DP arudi mezani kuchora karata ya 2022 kwani hurubaru imeanza matatizo

- Masaibu ya DP yalianza baada ya tofauti kati yake na Rais Uhuru Kenyatta ndani ya Jubilee

Naibu Rais William Ruto yuko pabaya kisiasa baada ya gurudumu la chama chake cha United Democratic Movement kutolewa pumzi.

Ruto na wandani wake walikuwa wameingia UDA baada ya moto kuwaka ndani ya Jubilee tofauti kati yake na Rais Uhuru Kenyatta zilipozuka.

Hata hivyo, paa la nyumba hiyo mpya pia limeanza kuvuja huku fito nazo zikibomoka na walio ndani kuhofia huenda haitaweza kustahimili kishindo cha 2022.

Ingawa DP Ruto hajatangaza kuondoka Jubilee, wandani wake wameweka wazi kuwa wanasubiri wakati murwa waruke nje.



UDA ilikuwa imeanza harakati kwa kishindo lakini duru zinaarifu chaguzi ndogo ambazo zimefanyika zimetilia shaka uwezo wa kuwika kwenye safari ya 2022.

Wagombea wa UDA kwenye chaguzi ndogo za Matungu, Kabuchai, Machakos na Naivasha walirambishwa sakafu.

Chama hicho kilifanikiwa kunyakua kiti cha MCA wa London kaunti ya Nakuru pekee baada ya kampeni kali zilizohusisha wandani wa DP kutoka Nairobi.



Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa ambaye amekuwa akieneza injili ya DP katika eneo la Magharibi ni mmoja wa wale ambao wamejitokeza na kusema 'mambo ni ngumu'.

Barasa alitangaza kuchukua likizo ya miezi minne kabla ya kuamua mkondo ambao atachukua kisiasa.

Mdadisi wa kisiasa Ambrose Weda alisema hatua ya Barasa ni mbinu ya kuondoka kambi ya DP Ruto baada ya kuona mambo ni mabaya.

"Tunatarajia watu waondoke, tutaskia mengi kama hayo. Hakuna kitu kama likizo kwa mwanasiasa mchanga ambaye bado ako sawa kama Barasa. Huyo ameondoka," alisema Weda.

Wandani wengine wa DP kama vile Bonny Khalwale ambaye amekuwa akipigia debe DP Ruto pia amehepa kwenye ulingo wa siasa.

Wadadisi wa kisiasa walisema siasa za Kenya huwa za kikabila na hivyo kumaanisha vigogo wa kijamii wana usemi mkubwa.

Hapo ndipo UDA imepata kibarua kupenya maeneo ambapo haina vigogo kwani wakazi wanafuata siasa za 'mtu wetu'.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke