Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuzo za MTV mama zaahirishwa

Diamond Pic Data Tuzo za MTV mama zaahirishwa

Fri, 5 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Nasra AbdallahMore by this Author Sherehe za utoaji tuzo za MTV Africa Music Awards (MAMAs) 2021 ambazo zilipangwa kufanyika katika mji mkuu wa Uganda Kampala zimeahirishwa.

Waandaaji tuzo hizo walitangaza jambo hilo jana Alhamisi Februri 4, 2012 kupitia mtandaao wao wa Twitter ambapo sherehe hiyo ilipaswa kufanyika Februari 20, 2021.

Kwa Tanzania wasanii waliokuwa wametajwa katika tuzo hizo ni msanii wa Bongo Fleva Zuchu aliyekuwa akiwania kipengele cha msanii chipukizi,  Diamond Platanumz aliyekuwa akiwania kipengele cha  msanii bora wa mwaka show kali kipindi cha  ‘lockdown’,

Wengine ni Harmonize aliyekuwa akiwania kipingele cha msanii bora wa kiume na Rostam walikuwa wakiwania kipengele cha kundi bora la mwaka.

Hata hivyo pamoja na tangazo hilo la kuahirishwa, MTV haikutoa sababu zozote za kwa nini wameamua  kukufanya hivyo.

Kufanyika kwa tuzo hizo Uganda,, ilikuwa ndio iwe mara ya kwanza kufanyika nchini humo na mara ya pili kufanyika katika  nchi za Afrika Mashariki.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz