Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Tutapigana hadi mwanajeshi wa mwisho' - Kiongozi wa RSF wa Sudan

'Tutapigana Hadi Mwanajeshi Wa Mwisho'   Kiongozi Wa RSF Wa Sudan 'Tutapigana hadi mwanajeshi wa mwisho' - Kiongozi wa RSF wa Sudan

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Kiongozi wa Kikosi cha Sudan Rapid Support Forces (RSF) amesema wanajeshi wake "wana uwepo mkubwa katika mji mkuu" na "watapigana hadi mwanajeshi wa mwisho" huku mapambano ya kikatili ya kupigania madaraka kati ya jeshi la serikali na RSF yakikaribia kuingia mwezi wake wa tano.

Katika ujumbe wa sauti uliotumwa kwenye mtandao wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter, Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo alirudia shutuma kwamba jeshi lilianzisha vita ili kuwawezesha washirika wa Rais aliyepinduliwa Omar al-Bashir kurejea madarakani.

Ujumbe huo ni mabadiliko kutoka kwa kauli yake ya tarehe 27 Agosti wakati kamanda wa RSF, ambaye anajulikana zaidi kama Hemedti, alitoa wito wa suluhu la mazungumzo na kuelezea mipango ya kurejesha serikali inayoongozwa na raia.

Hata hivyo, hatua hiyo ilikataliwa na mpinzani wake, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye amerudia kusema kwamba jeshi litaishinda RSF.

Jenerali Burhan amejitokeza mara kadhaa hadharani, ikiwa ni pamoja na ziara mbili za kigeni nchini Sudan Kusini na Misri tangu mwishoni mwa Agosti, akipendekeza kuwa jeshi lina uwezo mkubwa.

Serikali inayoongozwa na jeshi mara kwa mara imeitaka jumuiya ya kimataifa kutambua RSF, mshirika wake wa zamani, kama "shirika la kigaidi".

Wizara yake ya Mambo ya Nje ilisema mkutano wa hivi majuzi kati ya afisa wa RSF na mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki nchini Ethiopia ulikuwa "mfano mbaya".

Chanzo: Bbc