Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tutamtimua DP Ruto kutoka Jubilee muda ukifika, kwa sasa tunaomboleza Magufuli

34ec5f35cdad6358 Tutamtimua DP Ruto kutoka Jubilee muda ukifika, kwa sasa tunaomboleza Magufuli

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- NMC ya chama hicho hapo awali ilikuwa imechukua hatua ya kumuondoa Ruto kutoka wadhifa wa naibu kiongozi na kupeleka uamuzi huo kwa Kamati Kuu ya Kitaifa (NEC) inayoongozwa na Uhuru, ambaye angeamua hatima yake

- Walakini, baada ya mkutano mwingine wa NMC uliofanyika Jumatatu, Machi 22, Murathe alisema zoezi la kufukuzwa kwa Ruto limesimamishwa kwa heshima ya Magufuli

- Mbunge huyo wa zamani wa Gatanda alithibitisha kuwa bado wanashikilia uamuzi wao wa kutaka kiongozi naibu rais atimuliwe kutoka uongozi wa chama

Makamu mwenyekiti wa Chama cha Jubilee, David Murathe, sasa anasema muungano huo umesitisha kwa muda mpango wa kumuondoa Naibu Rais William Ruto katika uongozi wa chama ili kumuomboleza kwanza rais wa zamani wa Tanzania, hayati John Pombe Magufuli.

Kamati ya Usimamizi ya Kitaifa ya chama hicho (NMC) hapo awali ilikuwa imemtimua Ruto kutoka wadhifa wa naibu kiongozi na kupeleka uamuzi wake kwa Baraza Kuu la Uongozi (NEC) linaloongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, ambaye angetoa uamuzi wa mwisho.

Walakini, baada ya mkutano mwingine wa NMC uliofanyika Jumatatu, Machi 22, Murathe alisema zoezi la kumfukuza naibu rais chamani lilisitishwa kwa heshima ya Magufuli.

"Tumeweka kila kitu kwenye barafu kwa heshima ya Magufuli na kwa kuheshimu ushirikiano wetu na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kila kitu kimesimama hadi tutakapomaliza kuomboleza Magufuli,” alisema Murathe na kunukuliwa na The Standard.

Mbunge huyo wa zamani wa Gatanda alithibitisha kwamba NMC bado inashikilia uamuzi wake wa kuamuru naibu kiongozi kutimuliwa kutoka uongozi wa chama.

Yeye, hata hivyo, alisema kufukuzwa huko hakuhusiani kabisa na nafasi yake akiwa naibu rais.

Washirika wa Uhuru katika Jubilee walimshutumu Ruto kwa kutokuwa mnyenyekevu na uhusiano wake na chama cha United Democratic Alliance (UDA), chama tanzu cha Jubilee.

Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee, Raphael Tuju, pia alikuwa amefafanua kuwa, naibu rais ataendelea kutumikia nchi katika wadhifa wake wa sasa hata kama ataondolewa kwenye uongozi wa chama.

Akiongea na Spice FM Jumatano, Machi 17, waziri huyo asiyekuwa na majukumu alisema Ruto anaweza kufukuzwa kutoka wadhifa wa naibu rais ikiwa bunge litaamua kufanya hivyo.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Francis M Silva ni Mkuu wa Kitengo cha Kiswahili katika TUKO.co.ke. mwenye tajriba ya miaka mingi katika taaluma ya uwanahabari hasa uhariri - Radio, TV na Mitandaoni. Yeye ni zao la Chuo Anuwai cha Mawasiliano (KIMC). Amefanya kazi katika Radio Umoja, Good News Broadcasting System (GBS TV) na Idara ya Michezo ya Runinga ya Shirika la Utangazaji nchini KBC hadi leo. Hutumia tajriba yake kubwa katika kufanya iwe bora zaidi ya ilivyokuwa.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke