Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tutamlazimisha Ruto kuwapa Wakenya dili nzuri-Raila aapa

Tutamlazimisha Ruto Kuwapa Wakenya Dili Nzuri Raila Aapa Tutamlazimisha Ruto kuwapa Wakenya dili nzuri-Raila aapa

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: Radio Jambo

Kiongozi wa Azimio La Umoja-One Kenya Raila Odinga amesema maandamano yanayoendelea kote nchini yanafikisha ujumbe kwa utawala wa serikali ya Kenya Kwanza inayoongozwa na Rais William Ruto.

Akiwahutubia wanahabari katika ukumbi wa Jaramogi Oginga Odinga Foundation (JOOF) jijini Nairobi mnamo Jumatano,Odinga amesema Wakenya wengi wamelemewa na gharama ya juu ya maisha.

Kinara huyo amedai kwamba jana Jumanne usiku Azimio walipata dokezi za kuwepo kwa njama ya Kenya Kwanza kukomboa wakora kuwapiga risasi viongozi ambao wangejitokeza katika uwanja wa Kamukunji huku wakora hao wakilindwa na maafisa wa polisi.

“Ukweli ni kwamba maandamano kote nchini yanaonyesha wazi kwamba Wakenya wamelemewa na ugumu wa maisha,."

Kuhusu suala la uteuzi wa makamishna wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kiongozi huyo wa upinzani amesema ni sharti Dkt Ruto akubali majadiliano ya wazi ya wawakilishi kutoka Azimio na Kenya Kwanza kupata suluhu kwa maswala tata.

“Kwa umoja na ushirikiano tunaoonyesha, Ruto atakubali kuwapa Wakenya dili nzuri,” ameongeza.

Amewalaumu maafisa wa polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi na kuwaumiza waandamanaji ambao “kosa lao pekee ni kuonyesha wazi kutoridhishwa kwao na serikali ya Kenya Kwanza.”

Aidha,Odinga amesema hakuna kulegeza kamba hadi “Ruto aonyeshe yuko tayari kuwasikia Wakenya kujua matakwa yao na kuwaheshimu.”

“Ni sharti mjitokeze kutetea haki yenu kwa sababu Ruto akiachwa kusukuma mbele Sheria ya Fedha ya 2023 itakuwa ni kawauda kwa Wakenya kuteseka,” amesema Bw Odinga.

Anataka kiongozi wa nchi ajitokeze kuhakikisha vifungu tata vinang’olewa kwenye Sheria ya Fedha ya 2023 ili gharama ya maisha irudi chini.

Chanzo: Radio Jambo