Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Tuondolee Lockdown Kenya" Willy Paul amuandikia Rais Kenyatta

Screenshot 2021 04 18 At 02.41.07 660x400.png "Tuondolee Lockdown Kenya" Willy Paul amuandikia Rais Kenyatta

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Mwimbaji Staa wa Kenya Willy Paul amemuomba Rais wa Nchi hiyo Uhuru Kenyatta kuondoa lockdown iliyowekwa Nchini humo kwa lengo la kupambana na ugonjwa wa covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Sehemu ya aliyoyaandika Willy ni haya ——— > “Mr. President Wakenya walikuchagua kwa matumaini ya maisha bora na sio haya wanayoyapitia sasa hivi, kama kweli wewe ni Rais wa Watu ni muda wa kuonesha hivyo sasa hivi, unatarajia Wakenya wata-survive vipi wakati ‘umefunga’ Nchi?”

Nairobi. ( picture Kenya wall street)

“Tunataka kufanya kazi tutengeneze pesa tulishe familia zetu na tulipe bili zetu, tumechoka, bei zinapanda, gharama za maisha juu na wakati huohuo tunalipa mikopo na hatuna pesa, tafadhali fanya jambo” ——— Willy Paul.

Toka corona ianze kuitetemesha Dunia hadi sasa Kenya ina vifo vya Watu 2463, Wagonjwa wakiwa laki moja na elfu hamsini na moja na waliopona wakiwa ni laki moja na elfu moja, vifo vya dunia nzima kwa sasa vimefikia milioni 3 na elfu moja Wagonjwa milioni 140 na waliougua wakapona ni milioni themanini.

Chanzo: millardayo.com