Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tunisia yawazuia wahamiaji 69,000 kuingia Italia

Wahamiaji Watoto Wanachukuliwa Kama Watu Wazima Uhispania Tunisia yawazuia wahamiaji 69,000 kuingia Italia

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kipindi cha miezi kumi na moja iliyopita, Tunisia imezuia majaribio ya zaidi ya wahamiaji haramu 69,000 waliokuwa wanajaribu kuingia Italia kinyemela kutoka pwani ya Tunisia katika kipindi cha miezi 11 iliyopita.

Kituo binafsi cha redio cha Shems FM kimemnukuu Houcemeddine Jbabli, msemaji wa Walinzi wa Taifa wa Tunisia akisema hayo na kuongeza kuwa: "Wahamiaji haramu 55,200 kati yao waliokolewa kutoka kwenye boti zilizokuwa kwenye hatua za mwisho za kuzama, asilimia 55 kati yao walikuwa ni kutoka nchi mbalimbali za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara."

Mengi ya majaribio hayo yalizuiwa kwenye fukwe za jimbo la kusini mashariki mwa Tunisia la Sfax.

Pwani ya Sfax ni mahali pa kuanzia safari za magendo za wahamiaji wengi haramu wanaoelekea kisiwa cha Italia cha Lampedusa, kilichoko umbali wa kilomita 80 tu kutoka Tunisia.

Ingawa serikali ya Tunisia imechukua hatua kali za kukabiliana na tatizo hilo, lakini idadi ya wahamiaji haramu wanaoelekea Italia imekuwa ikiongezeka siku baada ya siku.

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu pia, serikali ya Tunisia ilitangaza kwamba imefanikiwa kuzima majaribio 52 ya wahamiaji haramu waliokuwa wanajaribu kuvuka bahari ya Mediterania kuelekeka barani Ulaya. Wahamiaji haramu wanaohatarisha maisha yao kwa tamaa ya kufika barani Ulaya kwa ndoto za alinacha za maisha bora

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia ilisema katika taarifa yake hiyo kwamba watu 1,004 wamekamatwa wakati wa operesheni ya kulinda usalama iliyofanyika katika kipindi cha Septemba 27 na 29 kwenye jimbo la kusini mwa nchi hiyo la Sfax.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Watunisia 216, wahamiaji 667 kutoka nchi za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara, na watu 73 kutoka mataifa mengine ni miongoni mwa watu waliokamatwa kwenye operesheni hiyo.

Kwa mujibu wa serikali ya Tunisia, zaidi ya wahamiaji haramu 37,000 walikamatwa mwaka 2022 wakati walipokuwa wanajaribu kuelekea barani Ulaya kupitia Tunisia, kinyume cha sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live