Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tunisia yakanusha kuwafukuza wahamiaji nchini

Tunisia Tunisiaaaaa Tunisia yakanusha kuwafukuza wahamiaji nchini

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Tunisia imekanusha madai kuwa imewafukuza kwa nguvu wahamiaji kutoka nchi za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia imesema: "Baada ya kuenea madai ya kulazimishwa kuondoka baadhi ya wahamiaji kutoka nchi ndugu za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara, Wizara ya Mambo ya Nje inathibitisha kwamba hakuna raia hata mmoja wa nchi hizo aliyefukuzwa kwa nguvu."

Wizara hiyo imesema kumesajiliwa baadhi ya maombi ya kurejea kwa hiari wakaazi wasio na kibali nchini Tunisia, maombi hayo yanachunguzwa na mamlaka husika hivi sasa na kwa kufuata taratibu za kisheria kikamilifu.

Wizara hiyo imesisitiza kuwa raia wa kigeni wana haki sawa ya kupata ulinzi nchini Tunisia na hakuna ubaguzi.

Wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa tarehe 21 Februari, Rais Kais Saied wa Tunisia alizungumzia wimbi la wahamiaji haramu kutoka nchi za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara na kuhimiza kukabiliana na wimbi hilo.

Saied alisisitiza kuwa, hali ya hivi sasa "si ya kawaida," na alitoa mwito wa kuchukuliwa hatua kali za kukomesha wimbi hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live