Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tunisia imezuia zaidi ya wahamiaji haramu 75,000 kuingia nchini Italia

Wahamiaji Haramu 75,000 Tunisia imezuia zaidi ya wahamiaji haramu 75,000 kuingia nchini Italia

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwaka 2023 Tunisia ilikamata zaidi ya wahamiaji haramu 75,000 walipokuwa wanajaribu kuingia barani Ulaya kupitia Bahari ya Mediterania na wengi wao ni wale waliokuwa wanaelekea Italia.

Hayo yameripotiwa na kituo cha redio binafsi cha Mosaique FM ambacho kimeongeza kuwa, mwaka 2022 mamlaka za Tunisia zilikamata mara mbili zaidi ya wahamiaji 35,000 wasio na vibali nje ya fukwe za nchi hiyo wakati walipokuwa wakisafiri kuelekea Italia.

Kituo hicho cha redio kiimenukuu ripoti ya msemaji wa Walinzi wa Taifa wa Tunisia, Houcemeddine Jbabli ambaye pia amesema, katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, maafisa usalama wa Tunisia wamezidisha operesheni za kukabiliana na mawimbi ya wahamiaji haramu wanaopelekwa katika kisiwa cha Lampedusa nchini Italia hasa kutokea mkoa wa kusini mashariki wa Sfax hadi mikoa mingine ya Tunisia.

Kisiwa cha Lampedusa cha Italia kiko umbali wa takriban kilomita 130 kutoka Tunisia. Mara nyingi kisiwa hicho huchaguliwa kama kituo cha kwanza cha wahamiaji haramu wanaofanya safari za baharini kuelekea barani Ulaya.

Mwanzoni mwa mwezi huu wa Februari pia mamlaka za Tunisia zilitangaza habari ya kusambaratishwa mtandao wa magendo ya binadamu ambao kazi yake kubwa ilikuwa ni kusafirisha kimagendo wahamiaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika kuelekea Italia.

Gadi ya Taifa ya Tunisia ilitangaza habari hiyo kwenye taarifa yake iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook na kuongeza kuwa, vitengo mbalimbali vya masuala ya kiusalama katika jimbo la Sfax la kusini mashariki mwa Tunisia vimefanikiwa kusambaratisha mtandao wa uhalifu uliokuwa unafanya biashara haramu ya magendo ya raia wa kigeni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live