Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tunisia imeruhusu kukamatwa kwa mgombea Urais mwaka 2009

Kabil Nabil Karoui, Mgombea Urais Tunisia

Thu, 2 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali nchini Tunisia, imeidhinisha hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa Mgombea Urais wa Taifa hilo 2019, Nabil Karoui na Kaka yake kwa kosa la kuvuka mpaka wa Nchi kwa njia haramu. Wawili hao wamekuwa kizuizini Nchini Algeria tangu Agosti 30, 2021.

Mbali na kushikiliwa wawili hao, imeelezwa kuwa mtu aliyewasaidia Viongozi hao kuvuka mpaka huo bila vibali ameshakamatwa na Polisi.

Kumekuwepo la wimbi la zuio la kusafiri na vifungo vya nyumbani dhidi ya Viongozi mbalimbali Nchini humo tangu Rais Saied alipovunja Bunge na kumfuta kazi Waziri Mkuu mwezi Julai mwaka huu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live