Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tunisia: Mahakama yawaachia huru wapinzani wa Rais

Tunisiaaaa Tunisia Rais Tunisia: Mahakama yawaachia huru wapinzani wa Rais

Sat, 15 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama nchini Tunisia imewaachilia huru wapinzani wawili mashuhuri wa kisiasa wa Rais Kais Saied, karibu miezi mitano tangu walipokamatwa kwa tuhuma za kupanga njama dhidi ya usalama wa serikali. Hayo yameelezwa na wakili wa wanasiasa hao Monia Bouali.

Chaima Issa na Lazhar Akremi wameachiliwa kufuatia kuwekwa vizuizini mwezi Februari pamoja na viongozi wengine 20 wa kisiasa katika operesheni ya kukandamiza wapinzani nchini humo. Wote wawili walishtakiwa kwa "njama dhidi ya usalama wa serikali".

Issa ni kiongozi wa Vuguvugu la Uokovu, muungano mkuu wa upinzani dhidi ya Saied ambao umeandaa maandamano dhidi yake katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Akremi, ni mwanasheria ambaye aliwahi kuwa waziri baada ya mapinduzi ya 2011 ya Tunisia na amekuwa mkosoaji mkubwa wa rais Saied.

Kabla ya jaji wa mahakama ya Tunisia kutoa uamuzi huo, jamaa wa familia nyingi za wafungwa waliandamana karibu na mahakama mjini Tunis, wakibeba picha za wafungwa hao na kutaka waachiliwe huru.

Maandamano ya kumpiga Kais Saeid Pamoja na hayo, jaji wa mahakama ya rufaa alikataa ombi la jopo la mawakili wa utetezi la kutaka wapinzani wengine wa kisiasa waachiliwe huru.

Vyama vikuu vya upinzani nchini Tunisia vinalalamikia kukamatwa viongozi wao vikisisitiza kuwa kuwekwa kwao kizuizini kunachochewa na sababu za kisiasa, huku mashirika ya kutetea haki nayo pia yakizitaka mamlaka husika ziwaachie huru watu hao.

Saied anayekosolewa vikali na wapinzani wake amewaita "magaidi" na wasaliti viongozi hao wawili wa upinzani walioachiwa huru na mahakama na kusema majaji wanaowaachilia watakuwa wanasaidia uhalifu wao wanaodaiwa kufanya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live