Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tunapendelea kupokea msaada wa kiufundi - waziri wa Libya

Tunapendelea Kupokea Msaada Wa Kiufundi   Waziri Wa Libya Tunapendelea kupokea msaada wa kiufundi - waziri wa Libya

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Wiki moja baada ya mafuriko makubwa kuharibu mji wa Derna, makundi ya uokoaji bado vinatoa maiti kutoka kwa majengo yaliyoharibiwa na baharini.

Waziri wa mambo ya ndani wa serikali inayojiita utawala wa mashariki - Essam Abu Zeriba - ameambia BBC kwamba ingawa wanakubali aina zote za misaada, kwa sasa wanapendelea "msaada wa kiufundi".

"[Sisi] tunapendelea kuwa na msaada wa kiufundi, yaani, timu za utafutaji na uokoaji na timu zilizobobea katika kutambua maiti. Libya haina uzoefu huo wa kiufundi," alisema.

Alizishukuru nchi ambazo tayari zilikuwa zikisaidia, zikiwemo Uturuki, UAE, Saudi Arabia na nchi jirani ya Misri.

Alisema timu zote zilisambazwa katika maeneo lakini alibainisha kuwa hii "ni kushuka tu kwa bahari ya maeneo yenye hali mbaya".

"Vikosi vyote vya uokoaji bado vinafanya kazi katika jaribio la kutafuta miili chini ya vifusi.

Pia kuna timu za uokoaji zinazofanya kazi baharini," aliongeza.

Maelfu ya watu wamefariki na wengine wengi bado hawajulikani walipo.

Chanzo: Bbc