Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tume ya uchaguzi Uganda yatishia kumuadhibu Museveni

190705133231 01 Yoweri Museveni File Super Tease 660x400 Tume ya uchaguzi Uganda yatishia kumuadhibu Museveni

Fri, 4 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Uganda Jaji Simon Mugenyi Byabakama, amesema kwamba tume hiyo haitasita kumchukulia hatua Rais Yoweri Museveni ambaye ni mgombea urais kupitia chama cha National Resistance Movement – NRM, endapo hatafuata sheria za kampeni zilizowekwa na tume.

Kulingana na tume ya uchaguzi, wagombea wanastahili kuandaa mikutano ya kampeni isiyozidi watu 200, na lazima wafuate maagizo ya maafisa wa afya ya kukabiliana na janga la virusi vya Corona.

Maagizo hayo ni pamoja na kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono, kuvaa barakoa na kutokaribiana.

Museveni amekuwa akifuata maagizo hayo na kuhutubia wafuasi wake kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, lakini katika siku mbili zilizopita, amehutubia umati wa watu ambao hawakufuata maagizo ya afya, katika wilaya za Busia na Bukedi.

“Tutamwandikia barua kumkumbusha kwamba anastahili kufuata maagizo yetu ili sote tupambane na janga la Covid-19, maagizo yetu hayana ubaguzi na usimamizi wetu wa kampeni hauna ubaguzi” Byabakama

“Unapoidhinishwa na tume ya uchaguzi kugombea nafasi yoyote, unakuwa mgombea wetu na lazima ufuate masharti yetu,” Byabakama

“Mwelekeo tuliotoa unatumika kwa kila mgombea. Museveni ni mmoja wao na anastahili kufuata masharti yetu. Kila mgombea anastahili kuhakikisha kwamba wafuasi wake ama mawakala wake wa kampeni wanafuata masharti hayo.” Byabakama

HARAKATI ZA SANGA JIMBONI, WACHANGA FEDHA KUTENGENEZA BARABARA, WALIA BEI YA MAZAO KUSHUKA

Chanzo: millardayo.com