Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tume ya Uchaguzi yakanusha kuhamisha wapiga kura

Kuraaa.png Tume ya Uchaguzi yakanusha kuhamisha wapiga kura

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya uchaguzi nchini Kenya (IEBC) imejitetea kuhusu kuhamishwa kwa orodha ya wapiga kura kabla ya uchaguzi wa urais kufanyika Agosti.

Tume ya uchaguzi imekiri kwamba kumekuwa na uhamishaji wa maeneo ya wapiga kura kinyume cha sheria, lakini imesema kuwa uchunguzi kuhusu suala hilo unafanyika.

Katika kipindi chote cha mwezi Mei, wapiga kura kote nchini wamekuwa wakithibitisha maelezo yao katika tume hiyo , shughuli iliyomalizika tarehe 2 Juni. Hatahivyo baadhi ya wapiga kura wamekuwa wakilalamika kuwa majina yao yamehamishiwa kwenye maeneo mapya ya kupigia kura bila idhini yao.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, anawalaumu maafisa wa usajiri katika majimbo 290 ya uchaguzi, na kaunti 47 kwa kufanya makosa ana akawaonya kuwa tume hiyo itachukua hatua dhidi wale wote waliohusika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live