Tume iliyoundwa na Rais Kenya kukagua utendaji kazi wa Shirika la Umeme la taifa la Kenya Power linalohitaji msaada wa kulipiwa deni la dola milioni 530 sawa na shilingi trilioni 1.22 za kitanzania limetoa mapendekezo kwa Hazina kuwezesha malipo hayo yaliyocheleweshwa kwa miaka miwili
Deni hilo ni mjumuisho wa fedha zilizokopwa kutoka kwa mashirika ya maendeleo ya kimataifa kama vile, China Exim Bank na Japan Development Bank ambao hadi sasa ndio walioidhinishwa na Serikali kulipwa fedha hizo.
"Tunatoa mapendekezo kwa Hazina kutoa kipaumbele kwa kulipa madeni haya kwani yamecheleweshwa kwa kipindi kirefu nje ya makubalianano" Imesema Tume hiyo.
Shirika hilo lilikopa kiasi cha dola milioni 129 sawa na bilioni 297.345 za kitanzania kutoka kwa China Exim Bank zilizopaswa kulipwa mwezi wa sita 2020.