Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tume ya Mawasiliano Uganda yavionya vyombo vya habari

Screenshot 2020 11 21 At 10.57.06 660x400.png Tume ya Mawasiliano Uganda yavionya vyombo vya habari

Sat, 21 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Baada ya kuripoti maandamano, Tume ya Mawasiliano nchini Uganda (UCC) imevitaka Vyombo vya Habari kuzingatia Kanuni na Taratibu hususan vinaporusha matukio mubashara.

Imesema, taarifa na matukio yanarushwa kwa namna ambayo inaweza kupotosha Umma huku ikitahadharisha kuhusu maudhui yanayoweza kuhatarisha Usalama wa Taifa.

Wanahabari wameelekezwa kutochapisha picha zenye maudhui ya kutisha ikiwemo vifo na majeruhi bila kutoa tahadhari kwa watazamaji.

Vyombo vya Habari vimekumbushwa kuzingatia Kanuni huku Mamlaka ikisema itawachukulia hatua wale watakaokiuka taratibu.

MATESO MAKALI ANAYOPATA MFUASI WA BOBI WINE, SABA WAMEUAWA

Chanzo: millardayo.com