Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tumba: Ufaransa haitaki kuwaondoa wanajeshi wake Niger

Tumba Jenenrali Niger Kikosi Tumba: Ufaransa haitaki kuwaondoa wanajeshi wake Niger

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Baraza la Kijeshi linaloongoza Niger ameeleza kuwa Ufaransa haina mpangp wa kuwaondoa wanajeshi wake mjini Niamey.

Jenerali Mohamed Tumba ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani katika Baraza la Kijeshi la Niger ameeleza kuwa, wameafiki muhula ulioainishwa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwa ajili ya kuwaondoa wanajeshi wa nchi hiyo huko Niger.

Jenerali Tumba ameongeza kuwa, Ufaransa inaunga mkono ugaidi nchini Niger na inaizuia nchi hii kunufaika na maliasili za nchi hiyo. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Niger ametahadharisha kwa mara nyingine tena kwamba Ufaransa haina lengo la kutekeleza uamuzi wa kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger. Viongozi wa kijeshi wa Niger

Baraza la Kijeshi la Niger pia wiki iliyopita lilitangaza kuwa jedwali za kuondoka wanajeshi wa Ufaransa nchini humo linapasa kutekelezwa kama ilivyoafikiwa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza mapema kwamba vikosi vya Ufaransa vitaondoka Niger ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Awali vyanzo vya habari vilitangaza kuwa kutokana na mkwamo wa kisiasa uliopo kati ya Paris na Niamey, baadhi ya rasilimali watu na nyenzo zinazohusiana na mapambano dhidi ya ugaidi zinaweza kuondolewa kutoka Niger.

Tarehe 26 Julai, 2023, vikosi vya ulinzi wa rais wa Niger vilimuondoa madarakani kiongozi wa nchi hiyo, Mohamed Bazoum, kwa tuhuma za rushwa, kushirikiana na nchi za Magharibi, na kutojali umaskini, na baraza la kijeshi likachukua utawala wa nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live