Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tukio la Ng'ombe kumuua mfanyakazi wa seneta lazua gumzo Kenya

Tukio La Ng'ombe Kumuua Mfanyakazi Wa Seneta Lazua Gumzo Kenya Tukio la Ng'ombe kumuua mfanyakazi wa seneta lazua gumzo Kenya

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: bbc

Fahali anayemilikiwa na seneta wa Kenya amemuua mtu anayemtunza katika kaunti ya magharibi ya Kakamega, na kuzua taharuki na huzuni katika eneo hilo.

Ng'ombe huyo wa thamani, anayeitwa Inasio, aligeuka na kuwa mkali na kumuua Kizito Moi, ambaye amekuwa akiwafunza fahali kwa zaidi ya miaka 20, Seneta wa kaunti ya Kakamega Boni Khalwale, mmiliki wa fahali huyo alisema.

Mwili wake uliokuwa na majeraha makubwa kichwani, shingoni, tumboni na mgongoni uligunduliwa Jumapili asubuhi.

Seneta huyo alisema alimuua fahali huyo kwa mkuki kulingana na mila za jamii ya Waluhya. Kisha nyama hugawanywa kati ya wanakijiji.

Bw Khalwale alisema ni nadra kwa wanyama kugeuka na kuwadhuru wanaowatunza, na kwamba kisa cha mwisho kama hicho kilitokea eneo hilo takriban miaka 30 iliyopita.

Fahali huyo mwenye umri wa miaka mitano, aliyekuwa na uzani wa kilo 120, alikuwa ametawazwa hivi majuzi kuwa bingwa.

Seneta huyo amekuwa akiandaa mashindano ya kupigana ya mafahali, maarufu sana magharibi mwa Kenya, ambapo maelfu ya wenyeji mara nyingi hujitokeza kushuhudia tukio hilo.

Wamiliki wa mafahali walioshinda kama Bw Khalwale wanachukuliwa kuwa mashujaa.

Chanzo: bbc