Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuju atembea kilomita 50 kwa mara ya kwanza tangu kuhusika kwenye ajali mbaya

5d59757165f3ab68 Tuju atembea kilomita 50 kwa mara ya kwanza tangu kuhusika kwenye ajali mbaya

Mon, 3 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Tuju anasherehekea hatua kubwa aliyopiga tangu kuhusika kwenye ajali ya kutamausha ambayo ilimuwacha amevunjika mifupa 18

- Katika video Tuju anaonyeshwa akiwa amevalia T-shirt, kaptula na jaketi akitembea kwenye maeneo ya milima bila usaidizi

- Katibu Mkuu huyo wa Chama cha Jubilee alihusika katika ajali ya barabarani akiwa safarini kwenda kuhudhuria mazishi ya Moi mnamo Februari 2020

Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee Raphael Tuju anasherehekea hatua kubwa aliyopiga tangu kuhusika kwenye ajali ya kutamausha ambayo ilimuwacha amevunjika mifupa 18.

Katika taarifa ya afisa wa mawasiliano wa chama cha Jubilee Polycarp Hinga, siku ya Jumapili, Mei 2, alifichua kuwa alifaulu kutembea kwa kilomita 50 bila tatizo.

Hinga alisema ni miujiza kwa Tuju kupiga hatua hiyo kinyume na mwaka jana.

Katika video ambayo ilipakiwa na Hinga kwenye kitandazi chake cha Twitter, Tuju anaonyeshwa akiwa amevalia T-shirt, kaptula na jaketi akitembea kwenye maeneo ya milima bila usaidizi.

"Mungu ni mkuu. Ikilinganishwa na nilipokuwa mwaka jana, namshuru Mungu. Asante kwa mchango wenyu na maombi wakati nilikumbwa na mshtuko wa ajali hiyo," Tuju alisema.



Itakumbukwa kwamba Tuju alihusika katika ajali ya barabarani wakati akiwa safarini kwenda Kabarak kwa mazishi ya marehemu rais mstaafu hayati Daniel Moi.

Gari la Tuju liligongana matatu Jumatano, Februari 12,2020, eneo la Kijabe wakiwa njiani kuelekea Nakuru.

Tuju aliyekuwa katika gari aina ya Toyota Prado alipata majeraha kifuani na sehemu ya tumbo huku dereva wake Austin Oindo akipata jeraha katika mkono wake.

Katibu Mkuu huyo wa Jubilee na walinzi wake walipata majeraha na wakakimbizwa katika Hospitali ya Misheni ya Kijabe kupata matibabu ya dharura.

Kisha baadaye alisafirishwa kwenda Nairobi Hospital kwa matibabu zaidi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke