Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Muhyiddin Yassin amekamatwa na Tume ya Kupambana na Ufisadi nchini humo, ikimtuhumu kwa mambo mbalimbali ikiwemo ubadhilifu katika mradi wa Jana Wibawa unaohusishwa na mabilioni ya dola.
Muhyiddin alikamatwa kwenye Makao Makuu ya Tume hiyo, baada ya kufika kwa mahojiano kuhusu kesi hiyo ya ufisadi inayoendelea dhidi yake ikihusisha fedha za kuwasaidia wakandarasi wa makabila ya Malay na makundi mengine, wakati wa janga la Uviko-19.
Kufuatia tukio hilo, Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini humo wamesema kukamatwa kwa Muhyiddin hakushangazi, lakini wakatahadharisha kuwa ni jukumu la serikali kuonesha kesi dhidi ya Kiongozi huyo na mpizani wa chama tawala si ya kisiasa.
Hata hivyo, taarifa ya tume Kupitia taarifa, tume hiyo imesema Muhyiddin atafunguliwa mashtaka hii leo Ijumaa Machi 10, 2023 chini ya sheria za ufisadi kuhusiana na mradi huo ambapo Waziri huyo zamani amekanusha madai hayo akisema yana ushawishi wa kisiasa.