Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshisekedi kwenda China kusaini mikataba ya kibiashara

Video Archive
Tue, 23 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, nchi yenye utajiri wa madini, Felix Tshisekedi, atafanya ziara nchini China kuanzia tarehe 24 hadi 29 mwezi Mei. Katika ziara hiyo rais Tshisekedi anatarajiwa kukutana na rais Xi Jinping ambapo atakagua na kusaini mikataba kadhaa muhimu ya kibiashara.

Mkutano utafungua njia kwa nchi hizo mbili kufanya marekebisho rasmi na kusaini mkataba na wawekazaji kutoka China wa dola bilioni 6 kwa miundombinu kwa ajili ya madini. Ziara hiyo ilitangazwa na wizara ya mambo ya nje ya China siku ya Jumatatu.

Tshisekedi aliagiza serikali yake wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri cha tarehe 19 mwezi Mei kuendelea na mazungumzo kuhusu makubaliano ya kibiashara na wenzao wa China baada ya serikali ya DRC na wadau wengine "kuimarisha msimamo wao," taarifa ya serikali ya DRC ilisema.

Aliwafahamisha wajumbe wa Baraza la Mawaziri kwamba kikosi kazi kinachoshughulikia mpango huo kimewasilisha mahitimisho yake, na kuwezesha majadiliano na washirika wa China kuanza katika siku zijazo.

Wakati wa ziara hiyo nchini China, wakuu hao wawili wa nchi watafanya mazungumzo na kuhudhuria hafla ya utiaji saini hati za ushirikiano, wizara ya mambo ya nje ya China ilisema.

"Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni nchi muhimu barani Afrika, na urafiki kati ya China na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ina historia ndefu," msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning alisema katika mkutano wa mara kwa mara na waandishi wa habari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live