Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshisekedi anavyoongoza kura DRC

Tshisekedi Na Fayulu Kupambana Tena Uchaguzi Wa Rais Wa DRC Tshisekedi anavyoongoza kura DRC

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CENI) imetoa matokeo zaidi ya awali ya uchaguzi wa Rais, yakionesha Rais Felix Tshisekedi anaongoza kwa mbali, akifuatiwa na Mfanyabiashara Moise Katumbi.

Mtandao wa DW_Kiswahili umeripoti kuwa matokeo yaliyotangazwa na CENI kufikia sasa yanatokana na takriban kura milioni 1.9, kati ya jumla ya wapiga kura milioni 44 waliojiandikisha katika nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati yenye ukubwa sawa na eneo la Ulaya Magharibi na yenye Wakazi zaidi ya milioni 100.

CENI imesema Tshisekedi mwenye umri wa miaka 60, aliye madarakani tangu 2019 na anayewania muhula wa pili wa miaka mitano, alikuwa anaongoza kwa zaidi ya asilimia 81 ya kura.

Alikuwa akifuatiwa kwa mbali na Mfanyabiashara tajiri na Gavana wa zamani wa Jimbo la Katanga Moise Katumbi, 58, akiwa na zaidi ya asilimia 15 ya kura na mtendaji mkuu wa zamani wa mafuta Martin Fayulu, 67, kwa zaidi ya asilimia moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live