Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshisekedi: Tumepoteza jabali, mtetezi wa mali za Afrika

163fe6b419146212bd3d1212a84df40a.jpeg Tshisekedi: Tumepoteza jabali, mtetezi wa mali za Afrika

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi amesema Afrika imepoteza jabali, na mtetezi wa uhuru na mali za bara la Afrika.

Tshisekedi ameyasema hayo katika viwanja vya Jamhuri Dodoma wakati akitoa salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha Hayati Rais John Magufuli.

Alisema, “Nimasikitiko makubwa yaliyojaa uzuni kwa ndugu yangu na rafiki yangu Magufuli msiba huu ni mzito, hauwagusi watanzania peke yake, kupotea na kuondoka kwa Dk Magufuli kumetingisha bara la Afrika .

“Afrika tumepoteza mwanasiasa mkongwe aliyelenbga kutetea na kulinda mali za Afrika na watu wake,” alisema Rais Tshisekedi na kuongeza;

“Tutabaki na kumbukumbu mpiganaji wetu na mzalendo wa kweli, sio tu kwa maslahi mapama ya watanzania bali ya umoja wa Afrika, mtetezi wa uhuruna bara la Afrika aliyekuwa analenga kutimiza ndoto za mshikamano za waasisi wetu wa bara la Afrika,”alisema

Katika hatua nyingine, Rais Tshisekedi amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan, kutorudishwa nyuma na wimbi ambalo limetokea kufuatia kifo cha Rais Magufuli.

“Wimbi lililosababishwa na kifo cha Dk Magufuli halitakiwi kupunguza spidi, mnapaswa kuendeleza dhamira yake, dira na kuendeleza aliyotamani kuyafanya kwa maendeleo ya taifa lenu…

“Hii ni fursa kwenu kuwa wamoja na kuleta maendeleo ya Tanzania, tunapoongelea dhamira ya Dk Magufuli nina pena kutaja mambo kadhaa ikiwamo mapambano aliyoanzisha dhidi ya ubadhilifu wa mali na kupambana na rushwa ambayo ni kansa ya muda mrefu iliyotafuna bara letu la Afrika.

Amesema pamoja na kuwahimiza Tanzania kuwa na msimamo ambao umekuwa wa kuigwa katika bara la Afrika pia amemtakia Rais Samia Suluhu Hassan mafanikio mema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz