Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshisekedi: Sitafanya mazungumzo na M23

Tshisekedi Aonya Mtafaruku Wa Maaskofu Tshisekedi: Sitafanya mazungumzo na M23

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwenye mahojiano maalumu na DW rais wa Kongo Felix Tshisekedi amesema kikwazo kwa amani katika kanda la Maziwa Makuu ni jirani yake rais wa Rwanda Paul Kagame.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amekutana mjini Berlin Jumapili jioni na rais wa Kongo Felix Tshisekedi na kuzungumzia hali ya kisiasa, kiusalama na kiuchumi nchini Kongo. Tshisekedi amewatolea wito wawekezaji kutoka Ujerumani kuwekeza nchini mwake.

Mkutano huo wa ana kwa ana baina ya Rais Tshisekedi na Kansela Scholz uliodumu kwa muda wa saa mbili ulifuatiwa na chakula cha jioni baina ya viongozi hao wawili. Taarifa ya ofisi ya Kansela Olaf Scholz imesema Ujerumani inaunga mkono juhudi za upatanishi wa mzozo wa Kongo zinazofanywa na rais wa Angola, Joao Lourencou. Mahusiano ya panda shuka na Rwanda

Kwenye mahojiano maalumu na DW, kando ya ziara yake, rais FĂ©lix Tshisekedi anasema yuko tayari kwa mazungumzo na rais wa Rwanda Paul Kagame, huku akitupilia mbali uwezekano wa mazungumzo na kundi la waasi la M23.

''Nimekuwa nikisema kila mara kwamba siwezi kamwe kukutana na waasi wa M23, sababu ni moja pekee : Ni vibaraka ambao walitengenezwa kwa ajili ya kuhalalisha uvamizi dhidi ya nchi yangu ya Kongo. Lakini kiuhalisia, mvamizi halisi, mhalifu halisi, ni Paul Kagame. Na ninataka kukutana naye sio kwa lengo la kumsihi au kujadiliana naye chochote, bali kwa ajili ya kumwambia wazi, ana kwa ana, kwamba yeye ni mhalifu, na lazima asitishe.", alisisitiza Tshisekedi.

Tshisekedi amesema anazingatia pia miito iliyotolewa na nchi washirika wa Kongo kwa ajili ya kuweko na usitishwaji mapigano ili kuipa nafasi juhudi ya kutafuta amani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live