Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshisekedi: Niko tayari kukutana na Rais Kagame

Rais Wa DRC Tshisekedi Anamlinganisha Kagame Wa Rwanda Na Hitler Tshisekedi: Niko tayari kukutana na Rais Kagame

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Felix Tshisekedi amesema kuwa, yuko tayari kukutana na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi hitilafu zilizopo baina ya mataifa hayo mawili jirani.

Hayo yamethibitishwa na Tete Antonio, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Angola ambayo ni mpatanishi wa Rwanda na DRC. Kwa mujibu wa waziri huyo, Rais Félix Tshisekedi amekubali kukutana na rais wa Rwanda, Paul Kagame, ikiwa sasa ni jukumu la upatanishi kufanyia kazi mkutano huo.

Idara ya mawasiliano ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pia inabainisha kuwa hakuna tarehe au eneo ambalo limepangwa kwa ajili ya mkutano huo iwapo utafanyika.

Mazungumzo kuhusu hali inayojiri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndio yaliogubika mkutano wa Luanda, hivi karibuuni kati ya Rais Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na mwenzake wa Angola Joao Lourenco, ambaye pia mpatanishi katika mgogoro huu. Marais wa DRC na Rwanda ambao nchi zao zimekuwa zikivutana kwa muda sasa na kutishia mustakabali wa uhusiano baina yao

Mkutano huu unafuatia mkutano mdogo ulioandaliwa Februari 18 kando ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia lengo likiwa ni kuwashawishi marais wa DRC na Rwanda kuketi kwenye meza moja ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zilizopo na kupunguza joto la uhasama unaoendelea.

Rais Felix Tshisekedi alisema hivi karibuni kwamba, yuko tayari kusitisha mpango wake wa kuanzisha vita na jirani yake Rwanda, ili kutoa nafasi kwa jitihada zinazoendelea za kupata suluhu ya mzozo unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikimtuhumu jirani yake Rwanda kuwa inaliunga mkono kundi la waasi wa M23, madai ambayo yanakanushwa na Kigali, lakini yanaungwa mkono na Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live