Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshisekedi: Mzozo Mashariki mwa DRC kuvuruga maandalizi ya uchaguzi

Tshisekedi: Mzozo Mashariki Mwa DRC Kuvuruga Maandalizi Ya Uchaguzi Tshisekedi: Mzozo Mashariki mwa DRC kuvuruga maandalizi ya uchaguzi

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: Voa

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi alisema Jumatatu kwamba mzozo na waasi mashariki mwa nchi hiyo unaweza kuvuruga maandalizi ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 20.

Tume ya uchaguzi ya Congo ilianza kuandikisha wapiga kura Februari 17 katika jimbo la Kivu Kaskazini, ambalo baadhi ya sehemu zake zinakaliwa na waasi wa M23, wanamgambo wanaoongozwa na Watutsi ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Congo kwa karibu mwaka mmoja.

Mapigano hayo yamesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao, jambo ambalo limezua wasiwasi kuhusu uwezo wa jimbo hilo kuandaa uchaguzi wa wabunge na rais baadaye mwaka huu.

“Kuendelea kwa vita mashariki mwa nchi yetu kuna kunahatarisha mchakato wa uchaguzi, ambao tayari unaendelea, kutokana na kuhama kwa watu wengi kutoka katika maeneo ya mapigano, ukosefu wa usalama na kutoweza kufikiwa kwa maeneo haya," Tshisekedi aliuambia mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu.

Chanzo: Voa