Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Troika ya SADC yaridhishwa mazingira ya uchaguzi

94cfca3e5d6b5f29e115d11c32ba7fe3 Troika ya SADC yaridhishwa mazingira ya uchaguzi

Thu, 22 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ASASI ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeridhishwa na mazingira ya hali ya siasa nchini Tanzania, kwamba yanaruhusu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Octoba 28,2020.

Imeeleza kwamba itaendelea kufuatilia mazingira ya uchaguzi huo.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi alisema TROIKA imekuwa ikifuatilia kwa ukaribu tangu awali mchakato wa uchaguzi hapa nchini na imeridhishwa na mazingira ya amani yaliyopo, hali inayoruhusu uchaguzi huo kufanyika.

Prof. Kabudi aliongeza kuwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipate uhuru kwamba uchaguzi huu unagharamiwa kwa fedha ya walipa kodi. Alisema maamuzi hayo yamefanyika kwa kutambua kuwa demokrasia ndio jambo kubwa katika uhai nautashi na kielelezo cha taifa ambalo ni huru kama ilivyo Tanzania.

Kuhusu waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi mkuu wa Octoba 28, Prof Kabudi alisema TROIKA imefanya tathimini ya awali ya hali ya usalama na kisiasa na kwamba Tanzania inategemea kuwapokea waangalizi kutoka Umoja wa Afrika (AU) na wale wa kutoka katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Katika tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi amepokea nakala za hati za utambulisho za Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Sarah Gordon-Gibson.

Katika mazungumzo yao, Prof. Kabudi alisema WFP imekuwa ni miongoni mwa mashirika ya kimataifa ambayo yana ushirikiano mzuri na Tanzania. Alisema mwaka 2018 WFP ilinunua tani 160,000 za nafaka na 2019 ilinunua tani 36,000 zenye thamani ya Sh bilioni 21. Fedha hizo zimesaidia wakulima wadogo katika kuboresha kilimo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa WFP, Sarah Gordon-Gibson alisema wamejadiliana namna ya kuendeleza ushirikiano baina ya pande hizo mbili, hususani kusaidia wakulima wadogo nchini kuboresha kilimo na kuboresha mazingira ya lishe.

Alisema kwamba shirika hilo lina mpango wa kuongeza msaada wanaoutoa kwa Tanzania.

Chanzo: habarileo.co.tz