Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Trilioni 2.2/- kuboresha miundombinu ya utalii Uganda

8c058a583095828da61187a80268471c Trilioni 2.2/- kuboresha miundombinu ya utalii Uganda

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WIZARA ya Utalii itatumia dola za Marekani milioni 600 (Sh trilioni 2.2) kuendeleza miundombinu ya utalii nchini kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Miradi mikubwa ya miundombinu ambayo serikali inakusudia kuendeleza ni Safu ya Milima ya Nile na Kagulu iliyopo Busoga, mradi wa maendeleo ya utalii ya Mt Rwenzori awamu ya II na mradi wa maendeleo ya utalii Mt Elgon.

Wizara imesema pia itaendeleza barabara kuelekea maeneo ya urithi wa kitamaduni wa Bigo, Byamugenyi, Nyero, Patiko na ngome ya Emin Pasha.

Pia imesema itaboresha uwanja wa ndege pembezoni mwa mbuga ya taifa ya Bonde la Kidepo, kujenga njia za maji ya baharini pamoja na gati 20 za kupandikiza Ziwa Victoria na Albert na kuboresha kilomita 370 za barabara za utalii kote nchini.

Barabara zitazoboreshwa ni ya kilomta 8 ya Kabale-Lake Bunyoyi, makao makuu ya Hifadhi ya Taifa Mgahinga ya kilometa 14, ya kilometa 54 ya Kisoro-Nkuringo-Rubuguri-Muko, kilometa 22 ya Rubuguri-Nteko na ya kilometa 88 Ishasha-Katunguru.

Nyingine ni barabara ya kilometa 149 ya Hamurwa-Kerere-Kanungu-Buleme-Buhoma-Butogota-Hamayanja-Ifasha-Ikumba, ya kilometa 184 ya Kitgum-Olumu-Kalenga-Kidepo-Kaabong na kilometa 117 ya Kebisoni-Kisizi-Muhanga-Kambuga.

Wakati akimtangaza balozi mpya wa utalii nchini mwanariadha Joshua Cheptegei anayeshikilia rekodi ya mita 10,000 hivi karibuni, Waziri wa Utalii, Tom Butime alisema uwekezaji huo unalenga kuongeza mvuto wa utalii na kuvutia wageni wengi.

"Uwekezaji huu utaongeza idadi ya watalii, thamani ya matumizi yao na hiyo itavutia uwekezaji ambao utaleta ajira zaidi ambazo zitaweka fedha nyingi mifukoni mwa Waganda," alisema.

Mpango wa Maendeleo wa Kitaifa (NDP III) una lenga kuwa, ifikapo mwaka 2025 watalii wa kimataifa wanaoingia Uganda kutoka Marekani, Ulaya na China wanaongezeka kutoka 210,000 hadi 500,000 na kuongeza mapato ya kila mwaka ya utalii kutoka dola za Marekani bilioni 1.

“Hii itaongeza mchango wa utalii kutoka asilimia 6.3 hadi asilimia 10 ambayo ni sawa na ajira mpya 433,000 na kuongeza jumla ya mchango wa utalii kwa Pato la Taifa kutoka asilimia 7.7 hadi asilimia 9,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz