Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Treni ya SGR yapiga breki za ghafla kuepusha kumfyatua jamaa aliyekuwa akikatiza

Train Mkl.jpeg Treni ya SGR yapiga breki za ghafla kuepusha kumfyatua jamaa aliyekuwa akikatiza

Sun, 18 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kisanga kilishuhudiwa kwenye reli ya kisasa ya SGR kati ya Nairobi na Suswa baada ya mwanamume mmoja kuonekana akitembea kwenye reli hiyo.

Katika video ambayo ilisambaa kwenye mtandao wa Twitter jioni ya Ijumaa, Septemba 16, treni hiyo ililazimika kusimama ghafla ili kuepuka kumgonga mwanamume huyo.

Katika video hiyo, wapiti njia walisikika wakisema kuwa hawajui jinsi mwanamume huyo alipofika eneo hilo lenye lililozingirwa na ua.

“Huyu si mfanyikazi. Hatujui alipandaje hapo, sisi tunamwona tu…na ni kama alilala hapo ndani. Jamaa alikuwa karibu asiagwe. Ni lazima ndege ikuje imtoe hapo,” mwanamke mmoja aliyeshuhudia kisa hicho anasikika akisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live