Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Togo yapiga marufuku maandamano leo

Drc Maandamano Vifo Togo yapiga marufuku maandamano leo

Thu, 11 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Togo imefuta maandamano yaliyopangwa ya siku tatu kuanzia leo ikisema mpango huo utavuruga utulivu wa umma katika taifa hilo la Afrika Magharibi ambalo limetawaliwa na familia moja kwa karibu miongo sita.

Waandamani wanapinga kukamatwa kwa viongozi wa upinzani na sheria mpya ya kufuta uchaguzi wa rais wakitaja kuwa ni kinyume cha sheria, hatua ambayo inaweza kuzidisha mvutano katika taifa hilo.

Wizara za Mambo ya Ndani na ile ya Usalama zilisema maandamano yaliyopangwa kufanyika wiki hii yatavuruga sana utulivu wa umma. Katika taarifa tofauti, serikali pia imesogeza mbele uchaguzi wa wabunge hadi Aprili 29, ikiwa ni wiki moja zaidi ya tarehe ya awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live