Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Togo yapiga kura ya wabunge

Togoooo Togo yapiga kura ya wabunge

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raia wa Togo wamepiga kura kuwachagua wabunge baada ya mageuzi ya kikatiba yaliyosababisha mgawanyiko ambao wapinzani wanasema yanampa Rais Faure Gnassingbe mwanya wa kuongeza muda wa kuendelea kushika madaraka.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa vituo vya kura vilifungwa mwendo wa saa kumi na mbili jioni na baada ya hapo kura zikaanza kuhesabiwa. Taarifa ya tume ya uchaguzi nchini humo ilikuwa imesema kwamba huenda matokeo ya awali yangelianza kutolewa jana jioni.

Makamu wakuu wa mikoa 179 wachaguliwa

Zoezi hilo ni la kuwachagua wabunge 113 na pia kwa mara ya kwanza, makamu wakuu wa mikoa 179 katika wilaya tano ambao pamoja na madiwani watachagua baraza jipya lililoundwa la seneti.

Kulingana na chama tawala chaGnassingbe, UNIR, hatua hiyo inaifanya Togo kuwa na uwakilishi zaidi lakini vyama vya upinzani viliwahamasisha wafuasi kupiga kura dhidi ya kile walichokitaja kuwa mapinduzi ya kitaasisi.

Baada ya kupiga kura hapo jana, Jean- Pierre Fabre, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, National Alliance for Change, alisema walikuwa na kampeini nzuri ya uchaguzi na kwamba wanalaani kasoro za uongozi uliopo madarakani huku akiongeza kuwa raia wa Togo watafanya maamuzi bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live