Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tofauti yazuka kati ya RSF na jeshi la Sudan kuhusu kusitisha vita kwa saa 24

Tofauti Yazuka Kati Ya RSF Na Jeshi La Sudan Kuhusu Kusitisha Vita Kwa Saa 24 Tofauti yazuka kati ya RSF na jeshi la Sudan kuhusu kusitisha vita kwa saa 24

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Kundi la wanamgambo la Sudan, Rapid Support Forces (RSF), limesema limejidhatiti kusitisha mapigano kwa saa 24 ili kuruhusu raia kupata misaada ya kibinadamu kwa usalama.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne, mkuu wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana zaidi kama Hemedti, alisema makubaliano hayo yamefikiwa kufuatia mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na "mataifa mengine rafiki".

"RSF inathibitisha tena kuidhinisha uwekaji silaha chini kwa muda wa saa 24 ili kuhakikisha kuwa raia wanapita salama na kuwahamisha waliojeruhiwa," Hemedti alisema.

Alilishutumu jeshi kwa kushindwa kuheshimu usitishwaji wa mapigano ya awali wa Umoja wa Mataifa, akisema wanajeshi hao wanadaiwa "kushambulia maeneo yenye wakazi wengi kutoka angani na kuhatarisha maisha ya raia".

"Hatua hizi ni ukiukaji wa wazi wa misingi na kanuni za sheria za kimataifa na za kibinadamu," aliongeza.

Hata hivyo ,Jeshi la Sudan limepuuzilia mbali madai ya wapiganaji wa kijeshi wa RSF kuhusu makubaliano ya siku moja ya kusitisha mapigano yamefikiwa, na kudai kuwa hizo ni propaganda tu.

"Hatujui uratibu wowote na wapatanishi na jumuiya ya kimataifa kuhusu usitishaji vita, na tangazo la waasi la usitishaji mapigano kwa saa 24 linalenga kuficha kushindwa ndani ya saa chache," msemaji wa Jeshi la Sudan alisema katika ukurasa wa Twitter wa Jeshi.

"Tumeingia katika hatua mbaya na juhudi zetu zinalenga katika kufikia malengo yake katika ngazi ya utendaji," taarifa ya jeshi inaongeza.

Milio ya risasi ilisikika mjini Khartoum mapema Jumanne asubuhi, huku idadi ya waliofariki ikikaribia 200.

Chanzo: Bbc