Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tishio kwa wapenzi wa jinsi moja Ghana: 'Tunaishi kwa hofu ya watekaji nyara'

Tishio Kwa Wapenzi Wa Jinsi Moja Ghana: 'Tunaishi Kwa Hofu Ya Watekaji Nyara' Tishio kwa wapenzi wa jinsi moja Ghana: 'Tunaishi kwa hofu ya watekaji nyara'

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Chuki kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja si jambo la kawaida nchini Ghana, ambapo mapenzi ya watu wa jinsi moja tayari ni kinyume cha sheria na yanahukumiwa kwa kifungo cha miaka mitatu jela, lakini sasa jumuiya hiyo ya LGBTQ+ inahisi hofu.

Mswada mpya, uliopitishwa na Wabunge wiki iliyopita, utaweka kifungo cha hadi miaka mitatu jela kwa mtu yeyote atakayejimbulisha tu kama anayeshiriki mapenzi ya jinsi moja au LGBTQ+ kwa ujumla na miaka mitano kwa kutangaza shughuli zao.

"Jamaa aliniambia ikiwa mswada huu utapitishwa, nafasi yoyote atakayenipata, atanitia sumu kwa sababu mimi ni chukizo kwa familia," Mensah, ambaye jina lake limebadilishwa ili kulinda utambulisho wake, anaiambia BBC.

Akiwa amevalia vazi jeusi kabisa, kijana huyo aliye katika umri wa mwisho wa balehe anaonekana kuwa na hofu kubwa: "Nina wasiwasi sana mtu yeyote anaweza kuniteka nyara hata katika majirani zangu wenyewe. Itakuwa vigumu sana kuishi hapa."

Amekuwa akiishi kwa muda na marafiki wanaomhurumia katika mji mkuu wa Ghana, Accra, tangu alipokosana na familia yake.

Haijulikani wazi jinsi jumuiya ya LGBTQ+ ilivyo kubwa nchini Ghana, taifa la kidini na la kimila, lakini wana mwelekeo wa kusaidiana wakati mmoja wao anakabiliwa na maisha kama mtu aliyetengwa.

Mensah anasema mama yake alipogundua miaka kadhaa iliyopita kwamba alivutiwa na wavulana, alianza kumpeleka makanisani kwa maombi akiwa na matumaini kwamba angebadilika.

"Hakuna marafiki isipokuwa marafiki zangu wa kanisa waliruhusiwa kuniona. Ilinibidi kujifunza Biblia 24/7, kuomba na ningekaa nyuma wakati wowote tunapoenda kwenye mikutano."

Anasema alikuwa akizuiliwa nyumbani - familia kubwa haikuzungumza naye na alipata sura yao isiyoweza kuvumilika."Walihisi ningekuwa na ushawishi kwa binamu zangu na watoto wadogo."

Chanzo: Bbc